Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, maandiko kamili ya tamko la Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Kielimu ya Qum Iran, katika kujibu kauli chafu za Trump dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
«وَإِنِّی لَأَظُنُّکَ یَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا»“Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia.”
(Al-Israa: 102)
Maneno machafu na ya ovyo ya Firauni anayetawala Marekani dhidi ya Ayatullah al-‘Udhma Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) yanatokana na asili chafu, duni na ya kishetani ya mtu huyu. Kauli hizi, kwa upande mmoja, zinaonesha kiwango cha juu kabisa cha kiburi na majivuno ya msemaji wake, na kwa upande mwingine zinaakisi udhaifu na unyonge wake mbele ya msimamo thabiti wa taifa la Iran, taifa ambalo daima lipo uwanjani.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Kielimu ya Qum inalaani vikali kauli zisizo na maana na zisizo na msingi za Rais wa Marekani mwenye dhana potofu, na inatangaza yafuatayo:
Katika kukabiliana na dharau au aina yoyote ya uchokozi dhidi ya heshima takatifu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, hatutakaa kimya kamwe. Sunna ya Mwenyezi Mungu ni kuwanusuru na kuwasaidia mawalii Wake, na ukweli wa historia umeonesha kwamba hatima ya wenye kiburi si chochote ila fedheha na udhalili;
“Hakika Mwenyezi Mungu humdhalilisha kila jeuri, na humwaibisha kila mwenye majivuno.”
Umma wa Kiislamu, ukiwa katika nafasi ya wafuasi wa Mtume Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake), ni “wenye nguvu dhidi ya makafiri” na utasimama imara hadi kutoa uhai wake kwa ajili ya kudumisha ahadi na mapatano yake na Naibu wa Imam (amani iwe juu yake).
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum Iran.
Maoni yako